MKUTANO MKUU WA SITA WA WANAHISA WA MWANGA HAKIKA BANK 2026

Jumamosi tarehe 9/5/2026, Derm Group kama mbia mkubwa (majority shareholder) wa Mwanga Hakika Bank, ilishiriki kikamilifu katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Wanahisa uliofanyika katika ukumbi wa Baobab Retreat, Mwanga Kilimanjaro.

Mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Ridhuan Mringo, na ulikuwa jukwaa muhimu la kutathmini mafanikio yaliyofikiwa, kujadili mwelekeo wa kimkakati wa benki, pamoja na kuimarisha dhamira ya pamoja ya kuendeleza ukuaji na ustawi wa Mwanga Hakika Bank.

Kupitia mkutano huu, wanahisa waliendelea kuthibitisha kujitolea kwao katika kuijenga benki imara, endelevu na yenye mchango chanya katika maendeleo ya uchumi.

Posted in
All

Post a comment

Your email address will not be published.